Web Analytics
KAGERE, MKUDE NA MORRISON KUCHUANA TUZO YA MCHEZAJI BORA SIMBA...


  • Explain

    Copyright © Sporty Leo

    KAGERE, MKUDE NA MORRISON KUCHUANA TUZO YA MCHEZAJI BORA SIMBA...

    SPORTYLEO MEDIA  LTD
    , November 29, 2021 WIB


     Nyota  watatu wa Simba SC Bernard Morrison, Jonas Mkude na Medie Kagere wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Novemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

    Kuchaguliwa kwa wachezaji hao kumetokana na uwezo mkubwa walioonyesha katika mechi tulizocheza Novemba.

    Awali walikuwa wachezaji watano akiwamo walinzi Joash Onyango na Mohamed Hussein lakini wamechujwa na Kamati Maalumu na kubaki watatu ambao watakaopigiwa kura na mashabiki.

    Zoezi la kupiga kura limefunguliwa leo na litafungwa Desemba Mosi saa 10 jioni ambapo atakayepata kura nyingi atatangazwa mshindi.

    Hassan Dilunga aliibuka mshindi wa mwezi Oktoba na kujinyakulia kitita cha Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini wa tuzo Emirate Aluminium ACP.

    Comments

    Show